Posts

Showing posts from March, 2017

YANGA vs AZAM KUTINGA UWANJANI HII LEO

Image
Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja ligi kuu Tanzania inaendelea leo kwa michezo miwili, ambapo Jijini Dar es salaam bingwa mtetezi klabu ya Yanga atakua dimbani kumenyana na klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC. Na hii hapa rekodi ya timu hizo katika mechi tano zilizopita za Ana kwa Ana za (VPL) Kati ya Miamba hii miwili, Azam FC wameshinda Mtanange mmoja huku mingine yote wakitoka sare.  Kwingineko Mbeya City itashuka dimbani kumenyana na Ruvu shooting.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEWASILI MCHANA HUU JIJINI DAR

Image

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI YA TAREHE 1 APRIL 2017

Image

Yanga yapata mtihani mzito

Image
KOCHA WA TIMU HIYO, GEORGE LWANDAMINA. KULEKEA kwenye mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Azam FC, benchi la ufundi la Yanga lipo kwenye mtihani juu ya kupanga kikosi chake kitakachokuwa na uhakika wa kupata ushindi. Yanga haitakuwa na huduma ya mabeki wake, Kelvin Yondani na Hassan Kessy ambao wote hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano. Mbali na hao, pia Yanga itamkosa mshambuliaji wake Mrundi, Amis Tambwe ambaye anauguza majeraha. Kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, aliiambia Nipashe kuwa hiyo ni changamoto kwa benchi lake la ufundi lakini wanapaswa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kesho wanaibuka na ushindi. "Bado kuna wachezaji wengine ambao wanaweza wakacheza kwenye namba husika, mambo kama haya yanatokea kwenye timu,huwezi ukawa na wachezaji wako wote wakiwa fiti kwenye baadhi ya mechi," alisema Lwandamina. Lwandamina alisema taarifa nzuri kwao ni kurejea kwa mshambuliaji wao, Donald Ngoma ambaye jana alitaraj

PICHA: Gari aina ya Lamborghini Huracan iliyozinduliwa kwa ajili ya trafiki wa Italia

Image
Kila nchi inatumia fedha nyingi kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi na raia wake lakini kuna nchi ambazo zimeenda mbali zaidi kwa kununua magari ya polisi ambayo mara nyingi tulizoea kuyaona yakitumika na matajiri kwenye matanuzi. Jeshi la Polisi nchini Italia limefanya uzinduzi wa gari aina ya Lamborghini Huracan kwa ajili ya kufanyia doria kwa askari wa barabarani ‘Trafiki’. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani Marco Minniti katika sherehe iliyofanyika Alhamisi March 30, 2017 ambapo miongoni mwa sifa za gari hilo ni pamoja na V10 engine, 610 horsepower, na kasi ya 0-62 hadi 3.2 kwa sekunde na kasi ya juu kabisa ni 201 mph (325 km/h).

Wakulima wa bangi wamshangaza DC

Image
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Godfrey Ngupula ameshangazwa na ujasiri walionao wananchi wanaolima mashamba makubwa ya bangi kwa kujiamini kama hakuna serikali. Akizungumza na wanahabari wakati akiwa kwenye operesheni ya kukamata na kuteketeza bangi,alisema baadhi ya wananchi wamegeuza hifadhi ya Igombe iliyopo mpakani mwa wilaya za Nzega kugeuzwa kuwa mashamba ya bangi. “Sijawahi kuona watu wanalima bangi kwa kujiamini kiasi hiki tena kwa wingi kama hakuna Serikali, tutahakikisha bangi yote inateketezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani,” alisema Ngupula Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nzega, Costantine Mbogambi alisema jeshi hilo litapiga kambi msituni kuhakikisha mashamba yote yanateketezwa.

Hizi ndizo faida ya kusoma nje ya nchi

Image
ASILIMIA kubwa ya Watanzania hupenda kwenda kusoma nje ya nchi jambo ambalo linaonekana kuwa ni la kawaida sasa. Hulka hii inatokana na ukweli kwamba fursa za kusoma katika nchi nyingine zinaweza kumfaidisha mwanafunzi pindi atakapofika katika nchi husika. Wanafunzi wanafursa ya kusoma katika nchi ya kigeni na kuona utamaduni na desturi za mazingira tofauti uliyoyazoea maishani mwao. Sababu muhimu ambazo zinaweza zikakufanya kwenda kusoma nje: KUIONA DUNIA Sababu kubwa unapaswa kufikiria kusoma nje ni fursa ya kuona dunia kwa maana kuwa ndani ya sayari ya dunia zipo nchi nyingi hivyo nafasi ya kusafiri kutoka nchi moja hadi nyingine ni fursa muhimu kwa binadamu yeyote kujifunza mapya tofauti na nchi aliyotoka. Hii itamsaidia pia kuchangamana na watu wenye mitazamo na desturi mpya. Lakini pia mbali ya kufaidi mazingira ya nchi unayojipatia elimu pia upo uwezekano wa kusafiri au kutembelea maeneo mengine wakati wa masomo yako, unaweza pia kutembelea nchi

CHEMICAL: SITASAHAU MAMA YANGU

Image
MSANII wa hip hop, Chemical amesema kila anapokumbuka kifo cha mama yake anajikuta akilia sana kutokana na kutamani angeyaona mafanikio yake ya sasa kupitia muziki wake. “Sikulelewa na mama yangu kwa asilimia kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, lakini nilipotimiza miaka mitatu nikaambiwa niende Dar es Salaam kumsalimia, nilifika na furaha kumbe ndiyo alikuwa amefariki, iliniuma sana ingawa nilikuwa na umri mdogo na kila mara huwa natamani angeyaona mafanikio yangu,” alisema Chemical. Chemical ni moja wa marapa walioibuka hivi karibuni pamoja na kufanya vizuri katika kazi zake nyingi pia ameleta changamoto kwa marapa wa kike waliomtangulia.