Posts
Showing posts from June, 2017
Mapengo ya waliokuwa na vyeti feki kuzibwa.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
VIBALI vya kuajiri watumishi wengine baada wengi kuondolewa kutokana na sakata la vyeti feki vinaendelea kutolewa ili kuziba mapengo yao. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaziba mapengo ya watumishi hasa wa afya walioondolewa kutokana na sakata la kuwa na vyeti feki. Majaliwa alisema ni kweli uhakiki umefanyika na serikali ikabaini kwamba baadhi ya wafanyakazi walikuwa na vyeti feki. Alisema wengine walikuwa na vyeti ambavyo ama vinatumika mara mbili kwa watu zaidi ya mmoja. “Lakini wapo waliobainika kwamba kuna utata katika majina katika vyeti hivyo, ambao ndio waliruhusiwa kukata rufaa na leo ndio siku ya mwisho ya kuangalia tatizo hilo,” alisema. Alisema baada ya uhakiki kukamilika, Rais John Magufuli tayari ameshatoa vibali vya kuajiri zaidi ya watumishi 50,000 na anaendelea kutoa na kinachoangaliwa zaidi ni kuziba mapengo ya watalaamu kwenye sekta mbalimbali.
Live ; Taarifa ya habari - Jambo Tanzania leo.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Zifahamu aina saba (7) za vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia
Aliyejaribu kufanya shambulio Msikitini akamatwa na Polisi
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Polisi nchini Ufaransa imemkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja. Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa. Mtu huyo hakuweza kutimiza azama yake baada ya kushindwa kuvipita vizuizi vilivyokuwepo mbele ya msikiti huo. Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia. Lengo la shambulizi hilo bado halijajulikana.
Trump na Putin kukutana uso kwa uso.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20). Itakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili. Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa. Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo. Source BBC SWAHILI.
LIVE ; Tazama hapa taarifa ya habari ya kutwa nzima ya leo
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
NAMFAHAMU MBWANA SAMATTA,MRISHO NGASA PAMOJA NA JUMA KASEJA. NI MANENO YA MCHEZAJI WA TOTTENHAM HOTSPURS.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama amesema kuwa yeye ni shabiki wa mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo kuliko Mfalme wa Barcelona, Lionel Messi. Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama Wanyama ambaye yupo nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza August 12 ambapo timu yake ya Tottenham ikiwa ugenini kuvaana na Newcastle. Ameyasema hayo kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na Radio Clouds FM. “Nawakubali wote wawili hawa ni wachezaji wa kubwa duniani na wakati mwingine naona kuwalinganisha ni ‘Unfear’ , lakini sababu mimi ni shabiki wa Madrid nasema Ronaldo, lakini hawa ni wachezaji wawili naona wako sawa, kwakuwa ni shabiki wa Madrid nasema Ronaldo. Wanyama alipo ulizwa ni wachezaji gani wa Tanzania ambao yeye anawafahamu hakusita kumtaja Mbwana Samatta.
MSUVA ; IMENIUMA KUONDOKA KWA NIYONZIMA ILA SINA JINSI.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amefunguka kuwa, kitendo cha Haruna Niyonzima kuondoka kikosini hapo, kimemuachia maswali mengi yasiyokuwa na majibu, hivyo ataendelea kummisi kila kukicha. Niyonzima ambaye msimu ujao ataitumikia Simba, ameondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba huku akishindwa kuongeza kutokana na kushindwana kimaslahi na viongozi wake hao wa zamani. Akizungumza na Championi Ijumaa,Msuva alisema, kati ya wachezaji wote wa kigeni aliowahi kucheza nao ndani ya Yanga, Niyonzima ndiye aliyetokea kuendana naye kwa kila kitu. “Kwa kweli Haruna nilimzoea kupitiliza, alikuwa kama mtani wangu, hivyo basi kwa hali hiyo iliyotokea, kwa upande wangu nimeumia sana lakini sina jinsi. “Kuondoka kwake haimaanishi kwamba nitashuka kiuwezo, bali nitaendelea kupambana na nitashirikiana na wengine kama nilivyokuwa nashirikiana naye.“Nitamisi vitu vingi kutoka kwake, najua hata yeye huko alipo nadhani anafahamu ameniacha kwenye hali gani, nasema hivyo kwa sababu
PICHA ; BEN POL AKUTANA NA EBITOKE LIVE.
- Get link
- X
- Other Apps
By
EBRO STATIONERY
-
Moja ya story kubwa ambayo ilimake headlines siku kadhaa zilizopita ni kuhusu Mchekeshaji Ebitoke kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda staa wa RnB Tanzania Ben Pol akimuomba waonane na ikiwezekana wafunge ndoa akisema anajitunza kwa ajili yake. Sasa leo June 23, 2017 kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake. “Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika? “Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo. “Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SA