Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuiunga mkono Marekani na jitihada zake za kupambana na mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini. Trump amesema kupata ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza Beijing kuhusu masuala ya biashara. Rais Donald Trump amesema aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka, mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un ''Rais wa China, Rais Xi, ninaamini amekuwa akimshinikiza pia.lakini mpaka sasa, pengine hakuna kilichotokea na pengine kimetokea. Hili lilikua kombora dogo, halikuwa kombora kubwa, halikuwa jaribio la Nuklia, ambalo alitegemewa kulitekeleza siku tatu zilizopita, tutaona nini kitakachoendelea'' Trump ametahadharisha kuwa mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni ya watu. Aliyasema hayo kwenye mahojiano na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya...