WASOMI WAZUA MJADALA ,KUHUSU VYETI FEKI

Wasomi wamepinga kufanyika kwa ubaguzi wa wenye vyeti feki kwa kuwaacha baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya katika uhakiki huo.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Rais John Magufuli kuagiza wafanyakazi 9,932 waliobainika kuwa na vyeti feki, waondolewe kazini.
Uamuzi huo wa Serikali umesaidia kunusuru kutumika kwa fedha nyingi kuwalipa watu wasiokuwa na sifa.
Kama watumishi hao wote wanalipwa kiwango cha kima cha chini cha mshahara cha Sh300,000 jumla ya Sh35.7 bilioni zimekuwa zikitumika kila mwaka kuwalipa.
Wakati akikabidhi orodha hiyo juzi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kazi hiyo haikuwagusa mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kwa kuwa wao wanatakiwa kujua kusoma na kuandika.
Kauli hiyo imeibua mjadala mzito kwa kile kilichodaiwa inalenga kutetea uovu na kuhalalisha mambo yasiyofaa bila kuangalia wakati uliopo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Bashiru Ally amesema licha ya kuwa kauli ya Kairuki ilitolewa kisheria lakini wakati umefika sasa kwa kuangaliwa upya kwa sheria hiyo ili watumishi wa Serikali wanaopatikana kisiasa nao wawe na elimu ya kutosha.
Amesema kwa waziri ambaye anasimamia masuala mbalimbali na kuwaongoza watu wengi walio chini yake ni kichekesho na aibu kueleza kuwa sifa kubwa anayotakiwa kuwa nayo ni kujua kusoma na kuandika.
Hoja hiyo pia imeungwa mkono na Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha ambaye amesisitiza ipo haja ya kuangaliwa upya kwa suala hilo kwani kuruhusiwa wanasiasa kuwa na vyeti feki ni hatari zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)