Posts

Showing posts from April, 2021

KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA PILI

Image
 KILIMO CHA PILIPILI KICHAA   Zao la pilipili kizao ni zao lingine ambalo limeanza kupata umaarufu katika soko la Dunia ambalo sasa litakuwa zao la ziada kwa wakulima wadogo kujiongezea kipato.Mmea huu hurefuka nakuweza kufikia urefu wa mita moja na nusu likitunzwa vizuri Zipo aina mbalimbali za pilipili kichaa lakini inayowika katika soko la dunia ni ile inayotoka Africa (African Bird's Eye Chilli) Pilipili kichaa toka Africa inaweza kuchanganywa na Mazao mengine kama kilimo mseto na Pia inaweza kulimwa kama zao la Biashara..Kwa kuanzia unaweza kulilima katika robo eka na kuendelea hadi hekta moja na zaidi  MASOKO Zao hili lina masoko ya ndani ya nchi na nje na ukuitaka kulilima unaingia mkataba na mnunuzi wa hapa nchini Tanzaniia na nje. MATUMIZI. Zao hili hutumika kama kiungo katika mboga.Kwneye mahospitali kwa tiba,Mabomu ya machozi., Kiuatilifu ya mazao mbalimbali pia hutumika viwandani kuzalishaa bidhaa mbalimbali. MAHITAJI KATIA UZALISHAJI WA MMEA HUU  Mwinuko...

KILIMO CHA PILIPILI KICHAA

Image
  UTANGULIZI Pilipili kichaa ni aina ya pilipili kali. Hustahimili hali ngumu ya  kimazingira na hazina magonjwa na wadudu wengi. Hali hii hufanya gharama ya ukuzaji kuwa chini zaidi kushinda mimea mingine. Pilipili kichaa ina wingi wa vitamin A na C na hutumika kama kiungo kwa chakula. Pia inaweza kukaushwa. HALI YA HEWA Huvumilia hali nyingi ikiwemo; joto na ukame ukizingatia unyunyizaji maji. Hata hivyo hali nzuri kwa mmea huu ni uvuguvugu na joto. Pia inahitaji mvua ya kadri kati ya 600mm – 1200mm kwa mwaka. Hali ya maji mengi mchangani hata kwa mda mchache husababisha kuanguka kwa majani. Pia upande mwingine ukame husababisha kuanguka kwa maua kwa hivyo nyunyiza maji. AINA YA UDONGO Hufanya vizuri katika aina tofauti za udongo, lakini zingatia usiwe udongo wa kutuamisha maji. Mmea huu hufanya vizuri unapotumia samadi. MBEGU Tumia mbegu iliyothibitishwa na kampuni ya MACE FOODS LTD. KUTAYARISHA KITALU Weka kitalu mita moja upana kwa urefu upendao kulingana na mbegu yako. E...