KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA PILI
KILIMO CHA PILIPILI KICHAA
Zao la pilipili kizao ni zao lingine ambalo limeanza kupata umaarufu katika soko la Dunia ambalo sasa litakuwa zao la ziada kwa wakulima wadogo kujiongezea kipato.Mmea huu hurefuka nakuweza kufikia urefu wa mita moja na nusu likitunzwa vizuri Zipo aina mbalimbali za pilipili kichaa lakini inayowika katika soko la dunia ni ile inayotoka Africa (African Bird's Eye Chilli) Pilipili kichaa toka Africa inaweza kuchanganywa na Mazao mengine kama kilimo mseto na Pia inaweza kulimwa kama zao la Biashara..Kwa kuanzia unaweza kulilima katika robo eka na kuendelea hadi hekta moja na zaidi
MASOKO
Zao hili lina masoko ya ndani ya nchi na nje na ukuitaka kulilima unaingia mkataba na mnunuzi wa hapa nchini Tanzaniia na nje.
MATUMIZI.
Zao hili hutumika kama kiungo katika mboga.Kwneye mahospitali kwa tiba,Mabomu ya machozi., Kiuatilifu ya mazao mbalimbali pia hutumika viwandani kuzalishaa bidhaa mbalimbali.
MAHITAJI KATIA UZALISHAJI WA MMEA HUU
Mwinuko
Humea vizuri katika mwinuko wa Mita 1500 toka Usawa wa Bahari.
MVUA
Humea vizuri katika mvua za wastani milimita 600 hadi 1200 kwa mwaka mvua ziki zidi hupukutisha majani na mizizi kuoza umwaagiliaji unahitajika ambapo hakuna mvua za kutosha'
JOTOPilipili huhitaji joto la kiasi cha nyuzi 20 hadi 30 ina unyevunyevu wa hewani wa wastani kukiwana na mgandamizo mkubwa wa hewa pilipili haitoi maua.
UDONGO
Udongo wa tifutifu wenye kiwango cha tindikali yani Ph ya 4.3 hadi 9.7 lakini utafiti unaonyesha humea vizuri kwenye p Ph 6.0 had 6.5.
MPANGO WA UZALISHAJI PILIPLI
1.Ingia mkataba na Mnunuzi kabla ya kuanzisha kilimo hiki ili uweze kuuza mara tu baada ya kuikausha
2.Pata mbegu sahihi toka kwa Wakala wako au mununuzi.
3Ukubwa wa shamba laoko uzingatie upatikanaji wa vibarua hasa wakati wa uvunaji.
4.Kilimo chako kizingatie kuwa isiwe pale ambapo ulikuwa umelima mazao ya kufanana nayo kama vili Bilinganya ,Nyanya,viazi mviringo,au tumbaku kwa mwaka uliopita.
MAANDALIZI YA VITALU
Pilipili ioteshwe kwanza kwenye vitalu kabla ya kuipeleka shambani
Tengeneza vitalu vya upana wa mita moja
Weka mbolea ya ngombe kama huna tumia mboji
weka mistari ya mbegu upana wa sentimita 10 kwalila mstari hadi mstariUkisha weka Mbegu weka udongo kiasi na weka nyasi kutunza unyevu nyevu na Mwagilia Maji mara kwa mara.
Mbegu zkiota toa nyasi na nyunyizia Dawa ya kuua wadudu na utunze mbegu ifike unene wa sentimeta 2-3 kwa urefu Sentima 8-10
Kiasi Cha Mbegu zinazohitajika
Gram 400 -500 zina hitajika kwa ekari mbili na nusu grm 20 zinatosha kutoa kiasi cha miche 500
UPANDAJI
Lima shamba lako na lilainishe kwa halo kama umetumia plau
NAFASI YA UPANDAJI
Mbegu zikiwa zimeshapata majani kati ya 4 hadi matano na urefu wa kati ya sentimita 8-10 mbegu zi hamishiwe shambani haraka na kupandwa kwa sentimta 45 mche hadi mche na 60 mtari hadi mstari na waeza kuweka zao lingine lisilo fanana nalo katikati iwapo ni zao laki biashara haishauriwi kuweka zao jingine kati yake
UWEKAJI MBOLEA
Inashauriwa kuweka tani 10 kwa hekta moja au kofi moja la mbolea kwa kila shimo mbolea ya samadi
Kilo 250kwa heta mbolea ya kupandi DAP auTSP au kiifuniko cha kiberiti cha box mche hadi mche na Mmea ukifikia sentimeta 15 au wiki 4 baada ya kupandikiza weka Mbolea ya CAN kilo 200 kwa hekta
WADUDU
Pilipili hushambuliwa sana na vidukari ,mchwa nzi weupe na kadhalika.
Fanya palizi ya mapema kuondoa maficho ya wadudu hao
Tumia vuatilifu kulingana na mdudu aliye shambuliwa kuzinga tia ushauri wa Bwana shamba
MAGONJWA
Pilipili ina magonjwa kama ya Ukungu,Kuvu sawa na magonjwa mengine ya nyanya Tibu mmea kabla haijapata magonjwa kwa kufuata ushauri wa bwana shamba.
MAVUNO
Pilipili huvunwa kwa kuchuma na huanza kuvunwa baada ya miezi 2-3 baada ya kuitoa kwenye kitalu na
huvunwa kwa mfululizo wa Miezi 3 hadi 4 na inashauriwa kuvuna kila baada ya wiki mbili
Isivunwe pamoja na vikonyo vyake na isivunwe ile mbichi ya kijani vuna iliyoiva na iliyopitiliza kuiva isivunwe
MAPATO
Shamba lilitunzwa vizuri kwa kila hekari moja ia uwezo wa kutoa kilo 1000 hadi 3000 kutegemea na utunzaji
BEI YA PILIPILI SOKONI
Kwa mwaka 2021 inakadiriwa kuwa na bei ya shilingi 5,500 _ 7,000/-kwa kilo moja
UKAUSHAJI BAADA YA KUVUNA
Huchukua muda wa siku 3 hadi 4 kukauka na isianikwe kwenye jua kali au kwenye unyevunyevu chini ikapoteza ladha kwa kupigwa na jua na kota kuvu inatakiwe isambazwe juu ya kichanja kilicho inuliwa na kukauka taratibu sio kwa kurundikwa
Usiweke kwenye gunia za sandarusi weka kwenye gunia za katani au kikapu ukiweka kwnye sandarasi huchemka na kuharibu ladha ya pilipili.
CHANGA MOTO ZA UZALISHAJI
Uvunaji ndio changamoto kubwa wa kilimo cha pilipili usipande kiasi usichoweza kukivuna
Panda kiasi cha pilipili ambacho unaweza kupata vibarua wakutosha katika uvunaji
USHAURI KWA WANAOTAKA KULIMA
Ingia mkataba na mnunuzi kwanza kabla haujaaanza kulima ndipo ukishafunga mkataba ndipo anza kulima
Kwa Mawasilaiano zaidi wasilia nami kwa
WhatsApp no 0627109810
Comments
Post a Comment