UTANGULIZI Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili 1. Faida za Parachichi upande wa Lishe Tunda lina vitamini zifuatazo Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu Madini- (Mineral Elements) Ni tunda lenye: Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxyge...