KILIMO CHA PARACHICHI.
UTANGULIZI
Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili
1. Faida za Parachichi upande wa Lishe
Tunda lina vitamini zifuatazo
- Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri
- Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve
- Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa
- Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili
- Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi
- Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu
Madini- (Mineral Elements)
Ni tunda lenye:
- Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi
- Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili
- Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili
2. Ustawi na Hali ya hewa
Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, (maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Tunduma, Njombe, Makete nk), linastawi vizuri sana, na huwa na fati nyingi
- Joto: Nyuzi 15-25 Sentigrade
- Muinuko: Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi
- Udongo: Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji
Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna aina za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika (mfano Tunduma, Kilimanjaro nk), parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno yake ni ya kawaida.
2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa Tanzania
i. Hass
- Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
- Ni tunda linalokuwa na vipelee vipele
- Limechongoka juu na chini
- Linahifadhika kwa urahisi
- Linafanya vizuri sana kwenye soko, hususani soko la nje.
- Kama unataka kuwekeza kwenye parachichi kwa ajili ya soko la uhakika basi HASS ni chaguo sahihi
ii. Aina ya pili ni Fuerte
- Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
- liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
- Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
- Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo
iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
- Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
- Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
- Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
- Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana
Upandaji wa Parachichi
Nafasi kati ya shimo na shimo
- Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
- Umbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7
Ukubwa wa shimo
- Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)
- Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90
Mbolea
- Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi: Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP
Kipimo cha mbolea,
- Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo
- Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc) kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa
KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
- Parachichi hasa hizi za kisasa, huanza kuzaa baada ya miaka 3 na matunda yake hukomaa baada ya miezi 6 hadi 12 tokea maua yanapotokea. Tunda la aina ya HASS ndilo huchelewa zaidi kukomaa huchukua kati ya mizei 7 hadi 12 tangu lilipo jitengeneza katika mti.
MAVUNO
- Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
- Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
- Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '
KIPATO na FAIDA
kwa kipimo cha mita 7 x mita 7, katika eka mmoja utakuwa na miti 80 hadi 100
- Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
- Hivyo kwa miti 80, utakuw na jumla ya matunda 80 x 1000= 80,000
- Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 80,000
- Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 80,000= 20,000,000tsh (MILIONI 20)
Kwa makadirio ya chini, unaweza kutengeneza milioni 20 kwa ekari 1 kwa msimu mmoj. Je Ukilima ekari 10, hapo tutazungumzia milioni 200. Kumbuka pia kilimo hichi hakina mambo mengi, hivyo si lazima kufika shamba kila wiki, unaweza kufika mara 1 kwa mwezi. Hii ina maana unaweza kulima parachichi huku unaendelea na mambo yako mengine.
Comments
Post a Comment