Trump aahidi umoja na mabadiliko kabla ya kuapishwa Marekani


Trump na Mike Pence wakiweka shada la maua makaburi ya taifa ya ArlingtonHaki miliki ya
Trump na Mike Pence wakiweka shada la maua makaburi ya taifa ya Arlington

Donald Trump ameahidi kuwaunganisha Wamarekani alipokuwa anawahutubia wafuasi wake wakati wa tamasha la mkesha wa kuapishwa kwake kuwa rais.

Akiongea katika vidato vya sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC, rais huyo mteule pia aliahidi kuleta mabadiliko.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo iliyodumu saa mbili ni mke na watoto wake, mwigizaji Jon Voight na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Soul Man, Sam Moore.

Bw Trump baadaye aliweka shada la maua katika makaburi ya taifa ya Arlington, Virginia.

Hafla hiyo ya Make America Great Again! (Fanya Marekani kuwa kuu tena) ilikuwa wazi kwa umma kuhudhuria na miongoni mwa waliotumbuiza ni nyota wa muziki wa country Toby Keith na Lee Greenwood.

"Tutaunganisha nchi yetu," Bw Trump alisema mwishoni mwa tamasha hilo.

"Tutaifanya Amerika kuwa taifa kuu tena kwa ajili ya watu wetu wote. Kila mtu, kila mtu, kote nchini. Na hii inajumuisha hata walio mitaa duni."

Wafuasi wake wamekuwa wakitiririka kuingia Washington DC, na aliwakumbusha kwamba kuna watu wengi ambao walidhani hangeshinda urais.

"Walisahau kuhusu wengi wetu,"alisema.

"Kwenye kampeni, niliwaita mwanamume aliyesahaulika na mwanamke aliyesahaulika. Naam, sasa nyinyi si watu waliosahaulika tena."


Trump na familia yake wakati wa tamasha

Bw Trump aliahidi kurejesha nafasi za kazi Marekani, kuimarisha jeshi na pia kuimarisha ulinzi mpakani.

"Mambo yatabadilika, nawaahidi. Mambo yatabadilika."

Alisema atafanya mambo ambayo hayajafanywa nchini Marekani mwa miongo mingi.

Mkewe Melania aliambia waliohudhuria tamasha hilo kuwa: "Kesho tunaanza kazi."

Bw Trump ataapishwa kuwa rais muda mfupi kabla ya saa mbili jioni saa za Afrika Mashariki (17:00 GMT) Ijumaa.

Bw Trump amewaomba maafisa 50 wakuu wa utawala wa Obama kuendelea kuhudumu hadi apate watu wa kujaza nafasi hizo.

Miongoni mwao ni mjumbe maalum wa Marekani kwenye muungano unaokabiliana na Islamic State Brett McGurk.

Mwingine ni naibu waziri wa ulinzi Robert Work.



Comments

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)