CHALINZE ; Watu 6000 kuajiriwa katika Kiwanda cha Vigae


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TIC), Clifford Tandari akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya uwekezaji wa viwanda uliofikiwa katika nchi naja jijini Dar es Salaam.

KIWANDA cha Vigae cha Twayfod kinatarajia kuajiri watu 4000 wa moja kwa moja na pamoja na ajira za muda mfupi 2000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini, Clifford Tandari amesema kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya Tanzania ya viwanda imeanza kutimia.
Tandari amesema kuwa wanaendelea kuchakata makampuni mbalimbali ambayo yameonyesha dhamira ya kutaka kuwekeza katika sekta ya viwanda hivyo ni fursa ya watanzania kuchangamkia ajira zinazojitokeza.

Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitakachojengwa katika mji wa Chalinze kitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ambapo kuna maeneo yatapata mapato yatayotokana na malighafi hizo.
Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitaanza hivi karibuni hivyo watu wakae tayari kuchangamkia fursa za awali ajira zitakazotolewa.

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)