Daraja La Bonyokwa-Kinyerezi lafunguliwa Rasmi na Meya wa Ilala
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million 478 hadi kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika.
Meya Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na kulitunza vyema daraja hilo kwani limejengwa kwa kodi zao.
Awali, Meya akitoa historia ya daraja hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa kujenga daraja hilo ni wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) lakini kutokana na kusuasua kwao, Mimi (Meya) niamua kuingilia kati kwa Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja la muda ili kuwasaidia wananchi wa Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa Kisiwa hususani wakati wa Mvua.
Comments
Post a Comment