Ibrahimovic ;kama sio Wanangu na Mourinho nisingekua Manchester United.
Ushindi huo umeifanya Man United kuwa timu yenye mafanikio zaidi kwa sasa.Baada ya mchezo huu mshambuliaji huyo wa zamani wa PSG alieleza mambo mengi ikiwemo suala la usajili wake na vile vile mafanikio aliyowapa United hadi sasa.Toka amekuja Man United Zlatan amekuwa kinara wa ufungaji akiwa amewapa United ngao ya hisani na kombe hilo la EFL.
Zlatan amesema mwanzoni hakuwa na uhakika kama atatua Man United.Zlatan amesema watoto wake walikuwa wanaizungumzia sana timu hiyo lakini pia simu ya kocha Jose Mourinho ilimshawishi kujiunga Man United.”Akili yangu haikuwa hapa lakini wanangu walianza kusukuma kuhusu hili,uhusiano wangu na Mourinho pia ulikuwa mzuri,inabidi United wamshukuru kwa hilo kwani alinipigia mwenyewe” alisema Mourinho.
Ibrahimovich ameeleza kwamba hajali kama United watafudhu katika Champions league msimu unao au laa.Amesisitiza kwamba yeye hakuja United kucheza UEFA bali ameipenda klabu hiyo na kama ni Champions League ndio sababu ya yeye kuja United,baasi asingekuja Man United kwani hata kipindi hicho anakuja United haikuwepo Champions League.
Baada ya ubingwa huo Zlatan ametupa dongo upande wa pili kwenye timu nyingine.Zlatan amesema yeye imemchukua miezi 7 kufanya kile ambacho timu nyingine zimeshindwa kukifanya ndani ya miaka 10 iliyopita.”Baada ya miezi 7 nina makombe mawili hapa,lakini timu zingine zimeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 10,ndani ya miezi michache hapa nimefanikiwa kufanya nusu ya kile ambacho baadhi ya timu imekifanya kwa miaka 10
Comments
Post a Comment