Madiwani wapinga kodi ya vitanda vya Gesti

Sakata la Tozo ya Kodi ya Kila Kitanda Nyumba za Kulala Wageni , baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Itilima wamekataa isitozwe na hivyo kuwepo mvutano uliodumu Takribani Masaa Mawili baadhi wakiunga Mkono ,hatimaye wameridhia kwa pamoja kukubali kodi hiyo japo kwa shingo upande, huku wapinga kodi ya Majengo isitozwe kwa kuwa mji huo una Makazi Holela.

Mvutano huo umetokea katika Baraza lililokuwa likipitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka 2017/2018 wakati wa mapendekezo ya makisio na matumizi , halmashauri ya itilima.

Pamoja na kuwepo kwa waraka kutoka Tamisemi ukielezea kuwepo kwa tozo hiyo madiwani waliendelea kutoitambua tozo hiyo wakidai inawakandamiza wafanyabiashara hao wa nyumba za kulala wageni na wengine pia wakapinga kodi ya majengo wakidai Itilima haina nyumba yenye hadhi ya kulipa kodi za majengo.

Makisio ya Matumizi ya Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2017/2018 Halmashauri inakadiria kutumia jumla ya shilingi bilioni 41 ikiwa ni Ruzuku ya Matumizi Mengineyo oc,mMshahara ,mapato ya ndani na miradi ya maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)