TFDA Yafafanua Kuhusu Dawa Yenye Virusi vya Machupo
Sabinus Paulo, Dar es salaam
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetolea ufafanuzi ujumbe unaosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna uwepo wa dawa za paracetamol zenye virusi vya Machupo ambavyo ni hatari endapo binadamu atatumia dawa hizo.
Katika taarifa ya TFDA iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu, imeeleza kuwa dawa aina ya P-500® (Paracetamol) inayotengenezwa na Apex Laboratories Private Limited ya nchini India haijaingia nchini Tanzania na haina kibali cha kungia.
TFDA inawatoa hofu Watanzania na kwa kutumia mifumo iliyopo itaendelea kufuatilia kwenye soko na mipakani ili kuhakikisha pamoja na bidhaa nyingine, dawa hiyo ambayo haijasajiliwa nchini haaiingiziwi bila kufuata taratibu.
Aidha TFDA imewaomba wananchi kuwa endapo watabaini na kuhisi kwamba dawa zozote walizozitumia zimewasababishia madhara wawasilishe taarifa kupitia njia ya kieletroniki ya www.tfda.go.tz/adr na TFDA itazifanyia kazi taarifa hizo.
Pia TFDA imewataka wananchi kuacha kusambaza jumbe zozote zenye taarifa zisizo rasmi na za kupotosha na kuogofya umma..
Comments
Post a Comment