Wenger amekataa dau nono la China


Arsene Wenger amekataa dau nono la pauni 30 milioni kwa mwaka ili kuhamia China.

Kwa mujibu wa taarifa za watu wake wa karibu zinadai kuwa bosi huyo wa Gunners angekuwa ni kocha anayelipwa zaidi duniani ikiwa ni mara mbili ya anachopokea kocha Pep Guardiola wa Manchester City.

Kwa mujibu wa jarida la Mirror, haikutaja klabu hiyo inayoshika Ligi Kuu China iliyoonyesha nia ya kumtaka Mfaransa huyo ambaye hatma yake Emirates bado ipo njia panda.

Wenger (67), amesema anataka kuendelea kufundisha soka katika klabu kubwa, lakini presha za mashabiki wa Gunners zinaweza kumfanya kwenda sehemu nyingine.

Kocha huyo wa zamani wa Monaco kwa sasa anapokea pauni 8milioni kwa mwaka katika mkataba wake wa sasa, lakini kuna kipengere cha kuongeza miaka miwili zaidi kama atapenda.

Wengers amejikutaka katika wakati mgumu baada ya Arsenal kufanya vibaya katika Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)