Leo tunakwenda kujifunza jambo muhimu sana ambalo wakulima wengi wa tikiti maji hua hawalifahamu au kama wanalifahamu hawalifahamu kwa kina ipasavyo. Ikumbukwe kwamba Hata ijapokua utafanya vizuri shughuli za shamba, kuna kigezo kikuu cha uzalishaji wa matikiti maji, ambacho kama usipokifahamu unaweza kupata hasara hata kama kila kitu umejitahidi kukifanya vizuri. Kigezo hicho ni UCHAVUSHAJI au kwa kitaalamu huitwa Pollination. Uchavushaji katika matikiti maji ni kigezo kikuu katika uzalishaji kitakachoamua wingi wa mavuno yako. Kwenye kilimo cha tikiti, Uchavushaji na utengenezaji wa Matunda ni sekta nyeti sana inayohitaji uangalizi wa hali ya juu. Ili kuelewa hili vizuri tutajifunza kidogo sayansi ya utengenezwaji wa maua ya mmea wa tikiti maji. Kwanza tuanze na kufahamu maana ya Uchavushaji. Karibu sana darasani. UCHAVUSHAJI (POLLINATION) Uchavushaji ni urutubishaji wa ua la kike la mmea kwa kutumia poleni (mbegu ya kiume) kutoka kwenye sehemu ya kiume ya ua la kiume. Mchakato
Comments
Post a Comment