LIMBWATA
HIVI USHAJIULIZA SIKU UKIPEWA LIMBWATA UKATELEKEZA FAMILIA, JE MKEO ANAWEZA KUHUDUMIA WANAO?
Msaidie mke wako kuwa Mama bora na mwanamke anayeweza kujitegemea, msaidie kusimama na miguu yake yeye mwenyewe bila kukutegemea wewe, msaidie kufanikiwa na kuweza kuyaendeleza mafanikio yenu. Wanaume wengi wanaogopa mafanikio ya wanawake, wengi huamini kua mwanamke akiwa na pesa anakua na dharau.
Ni kweli wakati mwingine mtu akipata pesa basi huwa na kakiburi flani, lakini hili si kwa wanawake tu hata wanaume. Ila kama mke wako akifanikiwa na kuwa na hako kakiburi lakini kumbuka kitu kimoja, mwanamke hata awe na kiburi kiasi gani lakini mwisho wa siku atakuja kuwa Mama kwa watoto wake. Kwamba anaweza kukufanyia kiburi wewe, anaweza hata kudai talaka na mkaachana.
Anaweza kupata mwanaume mwingine, lakini ni wanawake wachache sana, narudia wachache, wapo lakini ni wachache sana ambao hufikia hatua ye kutelekeza watoto wao kisa wamepata pesa. Hembu acha uoga na hata kama una moyo mgumu huwezi kumsaidia kwakua unampenda au kwakua unaona ni kitu kizuri hembu msaidie kwaajili ya watoto wako, mfanye awe bora ili kumuandaa na majukumu ya kulea wanao.
Maisha hayatabiriki, unapooa na kuamua kuwa na familia ni lazima ujiandae kwa leo na kesho, maana ya kesho ni kama Baba ni kuhakikisha wanao wanaishi vizuri hata kama wewe ukiondoka. Kwa maisha ya sasa unapaswa kujua kuwa hata kama unapendana vipi na ndugu zako lakini hawawezi kubeba jukumu la kulea wanao, ukiondoka mtu pekee atakayebeba hilo jukumu ni Mama yao ambaye ni mke wako.
Lakini hata kama kesho hutaondoka, kuna maradhi, hivi ushawahi kujiuliza kwa mfano ukaumwa ukalazwa hospitalini miezi miwili tu, je mke wako anaweza kuhudumia familia yenu au ndiyo mambo ya kwenda kuomba hela ya kula kwa ndugu. Lakini si hivyo tu, unachepuka, hivi ushajiuliza siku ukipewa limbwata ukatelekeza familia mkeo anaweza kuhudumia wanao? Hata kama humpendi mkeo hembu muandae hata kwa limbwata lako aweze kuhudumia familia! Lakini yatakuwa maajabu kama una MKE halafu humpendi itabidi ukapimwe akili.

Comments
Post a Comment