SHIDA YA KUWASIKILIZA WANAWAKE

SHIDA KUBWA YA KUTUSIKILIZA SANA SISI WANAWAKE ni kuwa ipo siku tutataka kutingisha kiberiti! Kama mwanaume ni lazima sana kuwa na kiwango cha kumsikiliza mwanamke wako!

Narudia, mpende Sana mke wako, mjali, mheshimu, mthamini sana lakini _usimsikilize kwa kila kitu_. Ni lazima uwe na mipaka na ni lazima uwe na uwezo wa kumuambia “Hicho kitu sitaki!” na akikuuliza sababu umuambie “Ni kwa sababu mimi ni mume wako na nimesema basi!”

Narudia, kama huna uwezo wa kumuambia mke wako hivyo basi jua kuwa atakukalia kichwani  hivyo ni lazima uwe na uwezo wa kumuambia mwanamke “SITAKI” hiyo ni kwa afya ya ndoa yako kwakua tu wanawake sisi tulivyo ukimpenda hivi kesho anataka zaidi, kesho kutwa zaidi na ukija kujishtukia basi unakuta mshachokana na ndoa ishakufa.

Wanawake tunaopendwa sana tunajisahau sana, tunaanza kujiona kama wanaume na kama sisi ndiyo tumeoa. Mtu upo kwenye ndoa unaanza mashariti shariti kibao kana kwamba umtoto wa darasa la pili! Sitaki hiki, sitaki kile, sipendi hiki sipendi kile, sitaki uongozane na flani sitaki sijui vile! Sitaki sitaki zinakua nyingi mpaka unashtuka hakutaki hata wewe, ni lazima kuweka mipaka ya sitaki sitaki zake kabla hajakupenda kichwani!

*Kaka zangu kama sauti haitoshi semeni spika zipo tunaweza kufunga mtaa Mzima!*

~Happiness

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KILIMO CHA TIKITI MAJI( WATER MELONY)