KILIMO: UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MOTONE
Ni matumaini yangu unaendelea vyema. Leo napenda kukuletea somo kuhusu teknolojia ya Umwagiliaji wa matone (Drip Irrigation) Umwagiliaji wa matone ni mfumo wa kisasa kwa umwagiliaji wa mimea na hasa mazao. Maji hupelekwa polepole kwa mabomba au mipira yenye matundu madogo moja kwa moja hadi kwenye shina laa kila mmea, karibu na mizizi yake. Mfumo huu unapunguza sana matumizi ya maji na pia shida nyingine mbalimbali Faida za umwagiliaji wa matone ni kama zifuatazo: Matumizi ya maji ni kidogo Mbolea za chumvichumvi zinaweza kuwekwa kupitia mfumo huu (fertigation), ambapo huchanganywa kwenye tenki la maji kisha kufikishwa karibu na mizizi, Maji yanapelekwa pale amboko mimea inayahitaji, siyo pale ambako hayaihitajiki Magugu yanapungua kwa sababu hayamwagiliwi (isipokuwa sehemu iliyo karibu sana na mazao) Hatari ya magonjwa wa fungus inapungua kwa sababu majani yanabaki makavu mfumo unahitaji pressure kidogo tu na hii inapunguza gharama za nishati (diseli, umeme) kwa ajili ya pampu hata