Posts

Showing posts from January, 2017

Picha: Meli kubwa ya kisasa ya Azam yatia nanga Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza

Image
Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga Bandari ya Tanga leo. Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki. Picha zaidi

Video; Hotuba ya Rais Magufuli nchini Ethiopia kwa kiswahili

Image
Jengo la amani na usalama lililopo makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia jana tarehe 29 Januari, 2017 limetangazwa rasmi kuwa litaitwa Mwalimu Julius Nyerere. Rais Magufuli alipewa heshima ya kutangaza rasmi kuanza kufanya kazi kwa jengo ==>Msikilize hapo chini akihutubia kwa Kiswahili

Jambazi auawa akijaribu kuwatoroka polisi

Image
MTU mmoja mwanaume ambaye amejulikana kwa jina moja la Mungiki (35) ameuawa kwa kupigwa na risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka baada ya kukutwa akiwa na silaha aina ya bastola yenye namba za usajili TZCAR 97076. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Januari 27, mwaka huu saa 6.30 usiku katika Mtaa wa Bwiru Kata ya Kitangiri katika Manispaa ya Ilemela. Alisema bastola aliyokamatwa nayo aliipora kwenye tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2013 mkoani Tabora. Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa kijana anayejihusisha matukio ya uhalifu wa kutumia silaha jijini Mwanza na mikoa jirani. “ Polisi walifanya ufuatiliaji wa tukio hilo, na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa na silaha hiyo na ndipo alipowaongoza askari hadi maeneo ya Songambele mtaa wa Kabohoro kwenye mapango ya mawe na kuikuta bastola hiyo ikiwa imefichwa kwenye pango la jiwe,”...

Wanaofanya biashara ya fedha bila leseni kukamatwa

Image
SERIKALI imetangaza kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola wafanyabiashara wa mitaani wanaokopesha fedha kwa riba bila kuwa na leseni ya biashara hiyo. Pamoja na wafanyabiashara hao, Waziri wa Katiba na Sheria Dk Harrison Mwakyembe ameomba wananchi wasaidie kuwafichua polisi na Mahakimu wanaowapa nguvu wafanyabiashara hao kinyume na sheria. Akizungumza na wanahabari jana mjini Iringa, Dk Mwakyembe alisema baada ya kuwasili mjini Iringa juzi kikazi aliwafuata akinamama watano waliolalamikia watu binafsi wenye fedha wanaofanya biashara hiyo ambao walilalamika kutozwa riba kwa mikopo wanayochukua jambo linalowatia umasikini. Dk Mwakyembe alisema kwa mujibu wa sheria namba 5 ya 2006 ni kosa la jinai kwa mtu yoyote kufanya biashara ya kukopesha fedha bila kuwa na leseni ya biashara hiyo inayotakiwa kulipiwa kodi. “Baada ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia, adhabu kwa mtu anayepatikana na kosa hilo ni ama kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shil...

Magazeti ya leo jumapili ya tarehe 29 january 2017

Image
Pitia vichwa vya magazeti ya leo

AZAM FC YAINYOA TENA SIMBA LIGI KUU

Image
Kipigo cha pili mfululizo ndani ya mwezi mmoja Simba wanapewa na Azam, baada ya Januari 13 kufungwa pia 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Goli pekee lililowekwa kimiani na nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bocco alifunga bao hilo dakika ya 70 baada ya kupata mpira mrefu wa mshambuliaji Mghana Mohammed Yahya na kumhadaa beki kisiki wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali kabla ya kumchambua kipa Mghana, Daniel Agyei.  Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo ndani ya mwezi mmoja Simba wanapewa na Azam, baada ya Januari 13 kufungwa pia 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar, bao pekee la Himid Mao.  Kipigo hicho kinapunguza matumaini ya ubingwa kwa Simba SC, iliyouanza vizuri msimu, kwani ikibaki na pointi zake 45 za baada ya kucheza mechi 20 inaweza kuenguliwa kileleni n...

Video ; Eric Omond how to do a Nigerian movie

Image

Watch the 8 type of animal robot you want to know

Image
High tecnology

Live; leicester city vs Barcelona friendly match

Image
LIVE MATCH WATCH HERE.

Here are the top 100 NHL players of all time

Image
LOS ANGELES — The list is in. And, as most expected, it’s wildly impressive. The NHL unveiled the full list of its 100 greatest players on Friday night, in a star-studded gala event at the Microsoft Theatre. Having earlier announced the first 33 ‘legends’ of the top 100 list — which included the likes of Gordie Howe and Maurice ‘the Rocket’ Richard — tonight, the league filled out the remaining 67 spots with a red carpet event, introducing players decade by decade. And here’s how it went. 1970s: Bobby Orr, Brad Park, Larry Robinson, Serge Savard, Ken Dryden, Tony Esposito, Bernie Parent, Bobby Clarke, Marcel Dionne, Phil Esposito, Jacques Lemaire, Stan Mikita, Gilbert Perreault, Jean Ratelle, Darryl Sittler, Yvan Cournoyer, Bob Gainey, Bobby Hull, Guy Lafleur. 1980s: Jari Kurri, Mike Gartner, Mike Bossy, Bryan Trottier, Peter Stastny, Denis Savard, Mark Messier, Pat LaFontaine, Wayne Gretzky, Ray Bourque, Paul Coffey, Al MacInnis, Denis Potvin, Borje Salming, Grant Fuhr,...

LIVE ; Dornald Trump akikabidhiwa utawala wa kuiongoza Marekani

Image
Tizama video hii live

Mahakama Kisutu yafuta kesi ya umeya Kinondoni

Image
Benjamini Sitta Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya matokeo ya umeya wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Mahakama imefuta kesi hiyo leo baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowekwa na meya wa manispaa hiyo, Benjamini Sitta kupitia kwa wakili wake, Baraka Nyambita. Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2016 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea umeya katika manispaa hiyo kupitia Chadema, Mustafa Muro na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya unaibu meya kupitia chama hucho, Jumanne Mbunju.

Simba, Yanga jino kwa jino

Image
Simba Yanga MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara zimeendelea kuwa za farasi wawili, Simba na Yanga baada ya matokeo ya katikati ya wiki. Jumanne Yanga ilipata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji Maji Maji kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na kuvunja mwiko wa kutoshinda dhidi ya timu hiyo kwenye uwanja huo kwa miaka 30. Wakati Yanga wakipata ushindi huo muhimu, Simba ililazimishwa suluhu na wenyeji Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya usiku wake Azam na wao kulazimishwa suluhu ya nyumbani na Mbeya City. Baada ya matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ingawa sasa ni kwa pointi mbili zaidi kutoka pointi nne dhidi ya Yanga kabla ya michezo hiyo. Simba wana pointi 45 na mabingwa watetezi, Yanga wana pointi 43 wakati Azam wamefikisha pointi 31 baada ya wote kucheza mechi 19. Simba inayofundishwa na Mcameroon Joseph Omog inataka taji la kwanza la Ligi Kuu tangu mwaka 2012, lakini ili...

Waziri Mwiguru Nchemba;Silaha za kivita,nyara za Serikali za sh milioni 131 zakamatwa Tabora

Image
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameshuhudia aina mbalimbali za silaha, zikiwamo za kivita 61 na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh milioni 131 zilizokamatwa hivi karibuni mkoani Tabora. Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa silaha na nyara hizo juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Seleman, alisema silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni maalumu iliyofanywa na polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Idara ya Maliasili mkoani hapa. Alisema operesheni hiyo, ililenga kupambana na majangili na wafanyabiashara haramu wa nyara za Serikali, baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanywa kistaarabu pasipo kutumia nguvu kubwa. “Silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni SMG 12, Rifle 6, Shotgun 2, magobole 41, risasi za SMG 47 na maganda yake matatu, maganda ya rifle matano na vichwa vya risasi za rifle vitatu. Alisema na nyara za Serikali zilizokamatwa zina thamani ya Sh milion...

Trump aahidi umoja na mabadiliko kabla ya kuapishwa Marekani

Image
Trump na Mike Pence wakiweka shada la maua makaburi ya taifa ya ArlingtonHaki miliki ya Trump na Mike Pence wakiweka shada la maua makaburi ya taifa ya Arlington Donald Trump ameahidi kuwaunganisha Wamarekani alipokuwa anawahutubia wafuasi wake wakati wa tamasha la mkesha wa kuapishwa kwake kuwa rais. Akiongea katika vidato vya sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC, rais huyo mteule pia aliahidi kuleta mabadiliko. Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo iliyodumu saa mbili ni mke na watoto wake, mwigizaji Jon Voight na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Soul Man, Sam Moore. Bw Trump baadaye aliweka shada la maua katika makaburi ya taifa ya Arlington, Virginia. Hafla hiyo ya Make America Great Again! (Fanya Marekani kuwa kuu tena) ilikuwa wazi kwa umma kuhudhuria na miongoni mwa waliotumbuiza ni nyota wa muziki wa country Toby Keith na Lee Greenwood. "Tutaunganisha nchi yetu," Bw Trump alisema mwishoni mwa tamasha hilo. "Tutaifany...

Jela miaka 7 kwa kujeruhi kwa panga

Image
MFANYAKAZI wa Kiwanda cha Jambo Plastic, Mustapha Juma (35) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kufanya kazi ngumu, baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi kwa panga Elias Charles na kumsababishia maumivu makali Juma, ambaye ni Mkazi wa Kurasini Dar es Salaam, alihukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi John Msafiri. Hakimu Msafiri alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka uliokuwa na mashahidi wanne. Alisema kuwa mshitakiwa huyo pamoja na kifungo chake, atatakiwa kufanya kazi ngumu kwa kuwa alimjeruhi mlalamikaji sehemu mbalimbali za mwili wake hususan kwenye kitovu na kumsababishia maumivu. Katika utetezi wake juu ya kwa nini asipewe adhabu kali, Juma, alidai kuwa ana familia inayomtegemea na hivyo kuiomba Mahakama hiyo kumpunguzia adhabu maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo. Inadaiwa kuwa Desemba 14, 2014 maeneo ya Vingunguti ndani ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, mshitakiw...

Serikali yakanusha uwepo wa mafua ya ndege nchini

Image
SERIKALI imesema hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa wa mafua ya ndege nchini. Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu mjini hapa jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hakuna mgonjwa yeyote aliyepatikana na ugonjwa huo nchini hadi sasa. Ummy alisema hayo akitoa ufafanuzi baada ya kuenea uvumi kwamba kisiwani Zanzibar, amepatikana mgonjwa mwenye mafua ya ndege. Alisema kutokana na kuibuka kwa ugonjwa huo nchi jirani serikali imetuma watalaamu mpakani mwa Tanzania na Uganda kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujihadhari na ugonjwa huo. Aliwataka madaktari wote nchini wakimwona mgonjwa mwenye dalili au mafua yasiyo ya kawaida, kumpima na kumpa tiba haraka kabla hajaugua au hajaambukiza.

Jenista Mhagama: satari ya dodoma iko palepale

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema ratiba ya kuhamia Dodoma kwa mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na manaibu iko palepale. Amesema watakaoshindwa kufanya hivyo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatoa mwongozo. Jenista alisema jana kuwa baada ya Februari 28, mwaka huu kutafanyika tathimini na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi, na kwamba kwa wale ambao hawatatekeleza agizo hilo, Waziri Mkuu Majaliwa atatoa mwongozo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Jenista alisema uamuzi ulitolewa na Rais John Magufuli uko palepale. Alisema hata Waziri Mkuu amekuwa akisisitiza ratiba ya kuhamia Dodoma kwa awamu ya kwanza Februari mwaka huu ambayo itahusisha mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao na baadhi ya watumishi wa wizara. "Kazi yetu itakuwa ni kuangalia utekelezaji utakuwa umefikia wapi na asiyetekeleza Waziri Mkuu atatoa mwongozo,” alisema Jenista. Pia ali...

Magazeti ya leo ijumaa ya tarehe 20 january 2017

Image