Posts

Showing posts from February, 2017

KITIMOTO ; chapigwa marufuku Rukwa

Image
Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo. Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi.  Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na kusambaa katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe. Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.

Urusi na China zatumia kura turufu kuisaidia Syria

Image
Urusi na China zimetumia kura turufu kuzuia jaribio la Umoja wa Mataifa la kutaka kuiwekea vikwazo serikali ya Syria. Marekani, Uingereza na nchi nyengine katika Baraza la Usalama, zilitaka kuiadhibu Damascus kwa tuhuma za kutumia silaha za sumu katika maeneo ya waasi. Ni mara ya saba sasa Urusi inatumia kura yake ya VETO kuikinga serikali ya Rais Assad na tuhuma za kimataifa. Katika hotuba yake iliyojawa hisia kabla ya kura, balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Matthew Rycroft, alisimulia kifo cha mwathirika mmoja ambae alipelekwa katika hospitali baada ya shambulio la gesi yenye sumu. Hata hivyo, kwa upande wake, balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Liu Jieyi, ameliambia Baraza la Usalama kwamba bado hakuna vilelezo kwamba serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali. Naye Rais Vladmir Putin amesema vikwazo vitazuia jitihada za mazungumzo ya amani yanayoendelea Geneva baina ya serikali na wapinzani wake. Marekani imesema Urusi na China zimeka...

Watano Mbaroni kwa kupatikana na dawa za kulevya

Image
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za Mvomero, Morogoro manispaa na Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na pikipiki maarufu kama boda boda. Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana na dawa hizo, wamekuwa na majibu tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo akidai ali...

Magazeti ya leo jumatano ya tarehe 01march 2017

Image

Live ; angalia hapa hotuba ya Rais wa marekani

Image

Highlight; Magoli kati ya juventus vs Napol (3-1)

Image
Mpira umemalizika na haya ni magoli yote yamchezo kati ya Juventus na napol  matokeo ni 3-1

Top 10 za nyimbo kali za wiki hii

Image
Hizi ndizo nyimbo kumi  zilizotikisa anga za majuu 

Diamond, Ali Kiba kuibeba Serengeti Boys

Image
Dar es Salaam. Wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz ni miongoni wa wajumbe wa kamati ya watu 10 wa kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania 'Serengeti Boys' Akitangaza kamati hiyo inayoundwa na wanahabari, viongozi wa kampuni na wasanii Waziri wa Habari, Utamaduni Sana'a na Michezo Nape Nnauye amesema jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo. "Tumeshamiria kuona timu hii inafanya maandalizi makubwa na nimeongea na Malinzi asubuhi hii yuko Morocco akiweka sawa masuala ya kambi ya vijana,"amesema. Kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanahabari mkongwe Charles Hillary na katibu ni katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine. Wajumbe wa kamati hiyo ni wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz wengine ni Beatrice Singano, Ruge Mutahaba, Maulid Kitenge, Erick Shigongo, Hassan Abbas na mwanamitindo Hoyce Temu. Serengeti Boys imefuzu kucheza fainali za vijana Afrika ...

SINGIDA; Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga mpaka kufa

Image
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu ...

CHALINZE ; Watu 6000 kuajiriwa katika Kiwanda cha Vigae

Image
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TIC), Clifford Tandari akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya uwekezaji wa viwanda uliofikiwa katika nchi naja jijini Dar es Salaam. KIWANDA cha Vigae cha Twayfod kinatarajia kuajiri watu 4000 wa moja kwa moja na pamoja na ajira za muda mfupi 2000. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini, Clifford Tandari amesema kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya Tanzania ya viwanda imeanza kutimia. Tandari amesema kuwa wanaendelea kuchakata makampuni mbalimbali ambayo yameonyesha dhamira ya kutaka kuwekeza katika sekta ya viwanda hivyo ni fursa ya watanzania kuchangamkia ajira zinazojitokeza. Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitakachojengwa katika mji wa Chalinze kitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ambapo kuna maeneo yatapata mapato yatayotokana na malighafi hizo. Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitaanza hivi karibuni hivyo watu wakae tayari kuchangamkia fursa z...

Serikali yabaini Bandari bubu ya dawa za kulevya

Image
Serikali imewaagiza watendaji wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanafanya operesheni maalum ya vyombo vya ulinzi na usalama katika eneo la bandari bubu ya Kigombe iliyopo pembeni mwa bahari ya Hindi,baada ya kubaini kuwepo kuwa eneo hilo ndio lango kuu la uingizaji dawa za kulevya,usafirishaji wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya kenya na uvuvi haramu wa mabomu. Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga,watendaji wa serikali pamoja na wananchi wa eneo la Kigombe,naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi mheshimiwa William Ole Nasha amesema ni lazima operesheni zifanywe kila wakati kwa sababu eneo la Kigombe limebainika kuwa ni kunafanyika uhalifu wa kimataifa ikiwemo kusafirisha binadamu kutoka nchi moja kwenda nyingine. Awali mbunge wa jimbo la Muheza mheshimiwa balozi Adad Rajab amesema mbali na uhalifu wa kimataifa kufanyika katika eneo la bandari ya Kigombe,pia vijana wengi wamekuwa wakitumia vyombo vya majini kusafiri na kwenda nje ya nchi na wanapofika huko ...

BARAKA ; Huyu ndio mfalme wa hip hop Bongo

Image
Msanii Baraka The Prince amefunguka na kusema rapa Lord Eyes kutoka Weusi ambaye pia ni msanii aliye chini ya usimamizi wake ndiye mfalme wa hip hop Bongo. Baraka The Prince amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV na kusema wasanii ambao wana 'diss' yeye kumsimamia Lord Eyes katika kazi zake ni wale ambao wanaogopa ujio wa rapa huyo katika muziki na kusema watu hao wanajua uwezo wa Lord Eyes hivyo kinawatisha kuona sasa anarudi. "Ukiondoa mimi kufanya biashara na Lord Eyes mimi ni shabiki wake namba moja, nimesikiliza ngoma zake nyingi sana unaona ni ngoma kali sana sema jamaa alikosa usimamizi tu wa kazi zake, nimesikia kuna watu wana 'diss' Lord Eyes kusimamiwa kazi zake na mimi nachoweza kusema hao ni waoga wanajua Lord Eyes ana talent kubwa hivyo wameanza kumuogopa, mimi namuona Lord Eyes ni mfalme wa hip hop Bongo" alisema Baraka The Prince

Daraja La Bonyokwa-Kinyerezi lafunguliwa Rasmi na Meya wa Ilala

Image
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.  Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam. Awali akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million 478 hadi kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika. Meya Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi wal...

Wazazi Wenye Watoto Wao ‘Panya Rodi’ Kukamatwa

Image
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, wilaya anayoiongoza ndiyo kitovu cha nchi kwa sababu ndipo yalipo makao makuu kubwa kuliko zote nchini kimadaraka, yaani Ofisi ya Rais Ikulu lakini pia wilaya yake ndiyo yenye pilikapilika nyingi za maisha kutokana na kuwa na biashara nyingi kubwa. Wahariri wetu hivi karibuni walifanya mahojiano naye ofisini kwake kuhusu mambo mbalimbali anayokabiliana nayo katika kazi zake za kila siku; ungana nasi: Swali: Tulipofika hapa katika ofisi yako tumekuta watu wengi sana wakisubiri kukuona, tatizo ni nini hasa? Jibu: Ni kweli watu wengi wanakuja kwa mkuu wa wilaya wakiamini kwamba kwa kuwa ni mwakilishi wa rais, basi watasaidiwa. Watu wanakuja na kero mbalimbali kuhusu ajira, maji, ulinzi, maisha mazuri na hakika nyingi zinakuwa hazijatatuliwa huko chini ndiyo maana mimi huwasikiliza wananchi kila Alhamisi nikiwa na wataalamu wa ardhi, barabara, maji na kadhalika. Kwa kawaida nimejipangia utaratibu, wananchi wanaanza kwenda kuonana na w...

Madiwani wapinga kodi ya vitanda vya Gesti

Image
Sakata la Tozo ya Kodi ya Kila Kitanda Nyumba za Kulala Wageni , baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Itilima wamekataa isitozwe na hivyo kuwepo mvutano uliodumu Takribani Masaa Mawili baadhi wakiunga Mkono ,hatimaye wameridhia kwa pamoja kukubali kodi hiyo japo kwa shingo upande, huku wapinga kodi ya Majengo isitozwe kwa kuwa mji huo una Makazi Holela. Mvutano huo umetokea katika Baraza lililokuwa likipitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka 2017/2018 wakati wa mapendekezo ya makisio na matumizi , halmashauri ya itilima. Pamoja na kuwepo kwa waraka kutoka Tamisemi ukielezea kuwepo kwa tozo hiyo madiwani waliendelea kutoitambua tozo hiyo wakidai inawakandamiza wafanyabiashara hao wa nyumba za kulala wageni na wengine pia wakapinga kodi ya majengo wakidai Itilima haina nyumba yenye hadhi ya kulipa kodi za majengo. Makisio ya Matumizi ya Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2017/2018 Halmashauri inakadiria kutumia jumla ya shilingi bilioni 41 ikiwa ni Ruzuku ya Matumizi Mengineyo oc,mMshahara ,m...

Wenger amekataa dau nono la China

Image
Arsene Wenger amekataa dau nono la pauni 30 milioni kwa mwaka ili kuhamia China. Kwa mujibu wa taarifa za watu wake wa karibu zinadai kuwa bosi huyo wa Gunners angekuwa ni kocha anayelipwa zaidi duniani ikiwa ni mara mbili ya anachopokea kocha Pep Guardiola wa Manchester City. Kwa mujibu wa jarida la Mirror, haikutaja klabu hiyo inayoshika Ligi Kuu China iliyoonyesha nia ya kumtaka Mfaransa huyo ambaye hatma yake Emirates bado ipo njia panda. Wenger (67), amesema anataka kuendelea kufundisha soka katika klabu kubwa, lakini presha za mashabiki wa Gunners zinaweza kumfanya kwenda sehemu nyingine. Kocha huyo wa zamani wa Monaco kwa sasa anapokea pauni 8milioni kwa mwaka katika mkataba wake wa sasa, lakini kuna kipengere cha kuongeza miaka miwili zaidi kama atapenda. Wengers amejikutaka katika wakati mgumu baada ya Arsenal kufanya vibaya katika Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Rekodi ya usaji wa Paul Pogba yaweza vunjwa na hawa

Image
Manchester United wana pesa,ni kati ya timu ambazo zikikamia kukuchukua zitakuchukua tu.Dunia haikuamini kiasi United walichokitoa kumrudisha Paul Pogba Old Trafford.Dau la £89m lilizitoa hata Barcelona na Madrid katika mbio za kumtaka Pogba.Lakini kocha wake Jose Mourinho anaamini siku sio nyingi Pogba anaweza azidiwe dau la usajilu na mchezaji mwingine.Hawa wafuatao kwa wanachokifanya sasa na hali zao klabuni wanaweza kuvunja rekodi ya usajili wa Pogba. Antoine Griezman(Athletico Madrid).Anaweza kufikia hata thamani ya £100m kwa sasa.Ni mchezaji watatu kwa ubora duniani akiwa nyuma ya Messi na Ronaldo,Griezman ameanza kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United,ameshawahi kukiri ugumu wa yeye kuhamia katika vilabu vya Hispania (Madrid na Barcelona).Lakini pesa za miamba hiyo miwili zinaweza kuvunja rekodi ya usajili aliyonayo Pogba kwa sasa.Kuwepo katika tatu bora ya Ballon D’or na mchezaji bora wa FIFA sio kitu kidogo na kinaweza kulifanya dau lake la usajili likawa ...

Ibrahimovic ;kama sio Wanangu na Mourinho nisingekua Manchester United.

Image
Manchester United wameweka kombe la kwanza kabatini kwao baada ya kuchukua kombe la EFL.Shukrani zimuendee mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovich aliyefunga magoli mawili kati ya matatu yaliyoipa ubingwa huo Manchester United.Ushindi huo wa Manchester United dhidi ya Southampton umewafanya United kuwa na jumla ya makombe 42 na kuipita Liverpool kwa idadi moja la kombe. Ushindi huo umeifanya Man United kuwa timu yenye mafanikio zaidi kwa sasa.Baada ya mchezo huu mshambuliaji huyo wa zamani wa PSG alieleza mambo mengi ikiwemo suala la usajili wake na vile vile mafanikio aliyowapa United hadi sasa.Toka amekuja Man United Zlatan amekuwa kinara wa ufungaji akiwa amewapa United ngao ya hisani na kombe hilo la EFL. Zlatan amesema mwanzoni hakuwa na uhakika kama atatua Man United.Zlatan amesema watoto wake walikuwa wanaizungumzia sana timu hiyo lakini pia simu ya kocha Jose Mourinho ilimshawishi kujiunga Man United.”Akili yangu haikuwa hapa lakini wanangu walianza kusukuma kuhusu hili,uh...

TFDA Yafafanua Kuhusu Dawa Yenye Virusi vya Machupo

Image
Sabinus Paulo, Dar es salaam Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetolea ufafanuzi ujumbe unaosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna uwepo wa dawa za paracetamol zenye virusi vya Machupo ambavyo ni hatari endapo binadamu atatumia dawa hizo. Katika taarifa ya TFDA iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu, imeeleza kuwa dawa aina ya P-500® (Paracetamol) inayotengenezwa na Apex Laboratories Private Limited ya nchini India haijaingia nchini Tanzania na haina kibali cha kungia. TFDA inawatoa hofu Watanzania na kwa kutumia mifumo iliyopo itaendelea kufuatilia kwenye soko na mipakani ili kuhakikisha pamoja na bidhaa nyingine, dawa hiyo ambayo haijasajiliwa nchini haaiingiziwi bila kufuata taratibu. Aidha TFDA imewaomba wananchi kuwa endapo watabaini na kuhisi kwamba dawa zozote walizozitumia zimewasababishia madhara wawasilishe taarifa kupitia njia ya kieletroniki ya www.tfda.go.tz/adr na TFDA itazifanyia kazi taarifa hizo. Pia TFDA imewataka wananchi kuach...

Mchawi, Huliwa Nyama Yake Guinea

Image
WAKATI ulaji wa nyama za watu ukitajwa kuwa hufanywa kutokana na matambiko maalum ya baadhi ya makabila nchini Papua New Guinea, kuna wengine wanasema ulaji upo kwa ajili ya dawa. Wapo wanaopinga kutokana na ukweli kwamba kuna wakati Wazungu saba waliliwa kwa mpigo kama tutakavyoona katika matoleo yajayo ya makala haya kiasi cha kusababisha serikali kushtuka na kuanza kuwasaka waliofanya kitendo hicho kibaya. Hakika ulaji wa nyama za watu siyo kwa ajili ya matambiko. Wakorowai ambao ndiyo kabila linaloongoza kwa kula nyama za watu nchini humo, vijana wao wanaochaguliwa kuingia katika kazi ya kuua, kukatakata nyama za watu na kuzipika, kwanza huchanjwa chale nyingi mwilini kwa kitu chenye ncha kali kisha kupakwa dawa. Vidonda hivyo vikipona huacha alama ambazo watafiti waliokwenda kulitembelea kabila hilo walizipa jina la tattoo japokuwa hizo ni chale. Wakati wa kuchanja chale hizo, kijana hufungwa kwa kamba mikononi ili asiwe na uwezo wa kumzuia mchanjaji wakati akifanya ...

Apigwa mpaka kufa baada ya kukutwa akifanya mapenzi na maiti ya mwanae

Image
Mwanaume mwenye umri wa miaka 45 kutoka Kenya amepigwa na Wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na maiti ya Mtoto wake aliyekuwa na umri wa miaka 15 ambapo ripoti ya K24 TV imeripoti tukio hilo kutokea kwenye kijiji cha Kiwanja Ndege kaunti ndogo ya Kuresoi Kaskazini.  Mashaidi wanasema baada ya mtoto kufariki kutokana na uvimbe wa Ubongo kichwani walihifadhi mwili kwenye chumba cha pekee lakini mida ya SAA nane usiku baba wa mtoto huyo aliamka na kwenda katika chumba hicho na ndipo alipokutwa akiwa anafanya mapenzi na maiti hiyo kitendo ambacho kiliwakasirisha wananchi na kuanza kumpiga hadi kupelekea kifo chake.

Hekari 1500 za RC Makonda Zazuiwa

Image
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemtikisa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuzuia ekari 1,500 za ardhi alizopewa na Kampuni ya Azimio Housing Estate (Ahel) na kusema kuwa ni mali ya Serikali. Uamuzi huo wa Serikali umekuja siku chache baada ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Iqbal kutangaza kumpa Makonda ekari hizo zilizoko katika eneo la Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni ili kuendeleza viwanda vidogo vidogo. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Lukuvi alisema Makonda alidanganywa kwa sababu wananchi walishashinda kesi mahakamani ambayo ilifunguliwa na Iqbal. “Eneo lile ni la Serikali si la yule mtu aliyejitangaza anampa Makonda na kwa sababu amemdanganya na mimi ndiye msimamizi wa ardhi, nitamsaidia Makonda kuchukua hatua ili watu wasijipendekeze kusafisha maovu yao kwa kutumia migongo ya viongozi. “Hadi siku ile (Jumanne iliyopita) alipokuwa anajipendekeza kwa Makonda, ardhi ile haikuwa yake, wa...

Hatimae Nyumba ya mama Wema yawekewa ulinzi mkali

Image
Nyumba ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu. Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa. Baada ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi. ”Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira” amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob. Meya alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegundua wanachama hao wa...

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limesema Uwanja wa kumbukumbu ya Namfua hauna vigezo

Image
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limesema Uwanja wa kumbukumbu ya Namfua ulioko mkoani hapa hauna vigezo vya kutumika katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akiukagua uwanja huo kwa lengo la kutoa maelekezo ya marekebisho yanayotakiwa kufanyika ili timu ya Singida United iliyopanda daraja iweze kuutumia. Madadi alisema ili uwanja huo uweze kutumika katika ligi hiyo ya juu nchini, itawalazimu wamiliki kuchukua vipimo upya na ushauri wa kiufundi wa matengenezo yanayohitajika ili wafanye ukarabati na kufikia viwango. “Lakini kubwa zaidi sehemu yenyewe ya kuchezea inahitaji kuboreshwa haraka na kuwekwa uzio kwa ndani, pia kuna haja ya kuwa na vyumba vya kubadilishia,” alisema Madadi. Katibu Msaidizi wa CCM Singida, Adamu Makulilo, alisema kuwa anaamini kwa kuunganisha nguvu za wadau wa soka mkoani hapa watakamilisha matengenezo yaliyoelezwa na hatimaye Singida United ikautumia katika mechi zake za nyum...

Nyavu zampeleka kizimbanimfanyabiashara

Image
RAIA wa India, Sheriaz Halari (56) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuhifadhi nyavu za kuvulia samaki zilizopigwa marufuku za thamani ya Sh milioni 427.7. Halari ambaye pia ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani leo mbele ya Hakimu Mkazi, Respicious Mwijage na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Mossie Kaima na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga. Kaima alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 17 (f) cha Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003. Amedai Februari 21 mwaka huu, maeneo ya Chamazi Msufini wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, mshitakiwa alikutwa amehifadhi mifuko 106 yenye vipande 6,042 vya vyavu za kuvulia samaki vya ukubwa usiopungua inchi tatu za thamani ya Sh milioni 422.9 ambazo zimepigwa marufuku kutumika nchini. Katika mashitaka ya pili, Kaima alidai kuwa Februari 21 mwaka huu, maeneo hayo ya ...

Serikali yafunga migodi Buhemba

Image
Butiama. Serikali imesitisha shughuli za kuchimba madini ya dhahabu katika migodi ya Buhemba na kuagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kulinda eneo hilo hadi Kampuni ya Taifa ya Madini (Stamico), itakapokamilisha uchunguzi wa usalama kwenye eneo hilo. Amri hiyo ilitolewa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa baada ya kutokea ajali ya pili katika migodi hiyo na kusababisha vifo vya wachimbaji wadogo wanne na huku wengine sita wakijeruhiwa. Amesema Serikali imefikia uamuzi huo ili kuepuka uwezekano matukio mengine ya ajali kutokea na kuendelea kugharimu maisha ya wachimbaji wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo. Usiku wa kuamkia Februari 13, mwaka huu, mgodi mwingine uliporomoka eneo hilo na kusababisha vifo vya watu watatu huku 15 wakijeruhiwa.

Highlight: magoli yaliyofungwa katika mechi ya jana kati ya liverpool na leicester city

Image
ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.

Zingatia Haya Kabla Ya Kufanyia Kazi Ushauri Wa Kibiashara Unaopewa

Image
Kama kuna kitu ambacho kila mtu anaweza kushauri kadiri ya utashi wake, basi ni ushauri wa kibiashara. Watu wengi wamekuwa wakipokea ushauri wa biashara unaotolewa na kila mtu, tena kwa bure, lakini wanapoufanyia kazi ndipo wanagundua haukuwa ushauri mzuri. Kila kipindi kuna aina za biashara ambazo huwa zinashabikiwa na watu wengi, biashara ambazo kila mtu anaongelea na wale wanaozifanya kuonekana waipata faida. Hapa ndipo unakuta kila mtu anashauriwa kuingia kwenye biashara hiyo, kwa sababu ndiyo ‘habari ya mjini’ kwa wakati huo na hivyo wengi wanakimbilia kuchukua hatua kabla fursa haijawapita. Changamoto nyingine kubwa inayowafanya watu kupewa ushauri ambao siyo makini kwenye biashara ni kutokuwa tayari kulipa gharama za ushauri. Wengi wamekuwa wakichukulia ushauri kama kitu kidogo ambacho hakipaswi kulipiwa. Hivyo wanachukua ushauri wa bure ambao unawaumiza sana. Leo tutakwenda kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanyia kazi ushauri wowote unaopewa kibi...

Watu wanne wapoteza maisha mgodi wa Buhemba

Image
Siku chache baada ya serikali kuufunga mgodi wa magunga uliopo buhemba wilayani butiama mkoani mara baada ya kuua watu wawili na kujeruhi 13, wachimbaji wengine wanne waliovamia mgodi huo katika shimo namba moja maarufu kama Long Base usiku wa kuamkia leo wanasadikiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi walipokua katika shughuli za uchimbaji wa madini kinyemela. Mpaka sasa tayari maiti mmoja imeopolewa huku zoezi la kuopoa miili mingine mitatu linaendelea pamoja na majeruhi saba wapo hospitali. Channel Ten ilifika katika eneo hilo na kazungumza na waokoaji pamoja na mashuhuda katika ajali hiyo na hapa wanasimulia. Masaa machache baadae kamati ya ulinzi na usalama mkoa ikafika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi. Kisha agizo likatolewa na mkuu wa mkoa linataka kufungwa kabisa mgodi huo huku eneo hilo likiwekewa ulinzi na askari wa jeshi la kujenga taifa.

Ndege za Israel zashambulia wapiganaji wa Hamas Gaza

Image
Ndege za kivita za Israeli, zimelenga maeneo kadhaa yanayoaminika kutumika na wapiganaji katika maeneo ya ukanda wa Gaza. Ripoti ya vyombo vya habari nchini humo, zinasema kuwa mengi ya maeneo hayo yaliyopigwa na mabomu, yanamilikiwa na vuguvugu la wapiganaji wa Hamas. Eneo moja linalotumika na wapiganaji wanaojiita Islamic Jihad, pia limepigwa bomu. Yamkini watu watatu wamejeruhiwa katika mashambulio hayo. Jeshi la Israeli limesema kuwa, mashambulio hayo ya hivi punde, ni kujibu kisasi cha kurushwa kwa maroketi kutoka Gaza hadi maeneo ya ndani kusini mwa Israeli.

Steve Nyerere, Mama Wema Wafika Pabaya

Image
DAR ES SALAAM: Hapatoshi na joto la ugomvi linazidi kupanda kila kukicha kufuatia mama wa mwigizaji Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu kuingia kwenye mgogoro mzito na Mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Wawili hao wameingia kwenye mgogoro huo baada ya Steve kumtuhumu mama Wema kuvujisha mazungumzo yao ya siri yaliyoshusha tuhuma nyingi kwa viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri. MUVI ILIVYOANZA Baada ya mazungumzo hayo ya siri kuvuja Alhamisi iliyopita, tathmini za wachangiaji mbalimbali mitandaoni, zilimmwagia lawama mama Wema kwa kuhusika na kusambaa kwa sauti hiyo kwani asilimia kubwa ya mazungumzo yaliyosikika katika ‘clip’ ya sauti hiyo, yalikuwa yakimuaibisha na kumfanya aonekane mmbeya mbele ya jamii hivyo isingekuwa rahisi Steve kuyavujisha. STEVE NAYE ANENA Siku hiyohiyo, Steve alizungumza na gazeti dugu na hili, Risasi Jumamosi ambapo alieleza kwa kifupi kuwa, mama Wema amehusika katika kuvujisha sauti hiyo ili amharibie maisha yake kwani mazu...